Saturday 7 February 2015

Tottenham Hotspurs yaipa kichapo Arsenal

Kane aigaragaza Arsenal, London Derby


Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane aliyefunga magoli mawili leo kwenye mechi yao dhidi ya Arsenal
Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane aliyefunga magoli mawili leo kwenye mechi yao dhidi ya Arsenal
Magoli mawili ya mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs yameipa timu yake ushindi mbele ya Arsenal kwenye mechi ya ligi kuu Uingereza iliyopigwa kwenye dimba la White Hart Lane.
Arsenal ndio walioanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa kiungo wao aliyetoka kwenye majeruhi ya muda mrefu Mesut Ozil goli lililofungwa dakika ya 11, lakini Harry Kane akafunga goli la kusawazisha dakika ya 56 na baadae akafunga goli la ushindi dakika ya 86 na kuipa ushindi timu yake.
Ushindi huo umeitoa Tottenham nafasi ya sita na kuipeleka mpaka nafasi ya nne nyuma ya Man United .

clouds stream