Thursday 26 February 2015

Chenge awasilisha utetezi Baraza la Maadili, hatma yake kujulikana kesho

Chenge awasilisha utetezi Baraza la Maadili, hatma yake kujulikana kesho

Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge.
Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge akitoka nje ukumbi wa Karimjee jijini Dares salaam mara baada ya kuhojiwa na tume ya Maadili.
Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge leo  amepandishwa  Baraza  la  Maadili   kwa kukiuka maadili ya viongozi wa umma, chini ya Tume  ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyoketi  jijini Dar es salaam.
Aidha, Andrew Chenge  miongoni mwa makosa anayokabiliwa nayo ni  ya ukiukwaji wa sheria ya maadili ya viongozi wa umma na alipokuwa  mtumishi  mkuu wa serikali kwa  wadhifa wa mwanasheria Mkuu wa Serikali AG,  alipitisha mikataba mbaalimbali dhidi ya  IPTL, na baadae alipostaafu nafasi hiyo ya Mwanasheria Mkuu  alikuwa miongoni mwa Washauri wakuu wa kampuni ya V.I.P Engineer.
Ambapo ilielezwa kuwa, Chenge hakuwahi kueleza tume hiyo ya Maadili kama ana madai ama ana hisa na kampuni hiyo ya V.I.P ambayo iliingia ubia na IPTL Katika uuzwaji wa hisa hali ambayo moja kwa moja ilipelekea kukiuka vifungu vya sheria.
Kufuatia  tuhuma hizo ,  Chenge aliweza kujitetea kwa  kuiwasilisha oda maalum ya utetezi wake dhidi ya madai anayodaiwa.
Mwenyekiti wa Baraza la Maadili    anayeshughulikia mashauri hayo  Balozi Jaji (Mst.) Hamisi Msumi alisema wataenda kukaa na kupitia oda hiyo ya Chenge na kisha watatoa maamuzi siku ya februari 26 mwaka huu ambayo ni kesho.
Katika hatua nyingine Baraza hilo la Maadili  kesho litaendelea tena  na shauri hilo la Chenge pamoja na viongozi wengine wa umma akiwemo aliyekuwa Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof.Anna Tibaijuka.

clouds stream