Thursday 12 February 2015

Misri: Kesi ya wanahabari 2 wa Aljazeera kuanza upya

Misri: Kesi ya wanahabari 2 wa Aljazeera kuanza upya

Waandishi wawili wa Aljazeera.
Waandishi wawili wa Aljazeera.
Mahakama ya Misri inatarajiwa hivi karibuni kuanzisha upya kesi dhidi ya wanahabari wawili waliokamatwa kwa kusaidia vuguvugu la Muslim Brotherhood.
Mohamed Fahmy na Baher  Mohamed  wanafanyia kazi televisheni  ya  Al-Jazeera  yenye makao yake Qatar. Walihukumiwa miaka kumi Jela na mwenzao wa Australian , Peter Greste.
Greste aliachiliwa juma lililopita kutokana na sheria mpya inayoruhusu kuwarejesha kwao raia wa kigeni waliofungwa Misri.
Kusikizwa kwa kesi hiyo tena kuliagizwa na mahakama ya rufaa ambayo ilitaja uamuzi wa mahakama iliyosikiza kesi hiyo kuwa uliofanywa ovyo bila kuzingatia ushahidi.

clouds stream