Saturday 7 February 2015

Fainali AFCON: Bingwa kujulikana leo


Fainali AFCON: Bingwa kujulikana leo



Andre Ayew (kulia), Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Ghana
Andre Ayew (kulia), Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Ghana
Leo ndio fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON ambapo miamba miwili ya soka barani Afrika inakutana kuchuana vikali kumtafuta bingwa mpya wa michuano hiyo mikubwa kwa upande wa soka inayofanyika nchini Equatorial Guinea.
Upande mmoja kuna kukosi cha nyota wengi wa Afrika kwenyeb timu moja kuwahi kutokea ‘golden generation’, wakati kwa upande wa pili Ghana wao kikosi chao kinaundwa na kundi la wachezaji wengi ambao walitwaa ubingwa wa dunia 2009 kwa vijana wa umri chini ya miaka 19 ‘U-20 World Cup.
Kama asingikua mshambuliaji wa Urugua na klabu ya Barcelona Luis Suarez kuunawa mpira uliokua unaelekea golini, basi leo Ghana ndio ingekuwa timuu pekee ya Afrika yenyen mafanikio katika fainali za kombe la dunia kwa kua timu ya kwanza kutinga hatua ya nusu fainali za michuano hiyo mikubwa duniai kwa mchezo wa mpira wa miguu.
Lakini kwa upande wao Ivory Coast pamoja na majina makubwa yaliyo katika timu yao, wameshindwa kuonesha makali yao kwenye michuano mbalimbali ikiwemo ya ndani ya Afrika na hata ya ile ya nje ya Afrika.
Kwa mara ya kwanza bila ya mchezaji wao maarufu Didier Drogba ambaye amekitumikia kikosi hicho kwenye mashindano tangu mwaka 2002, walionekana kutokua na matarajio ya kutwaa ubingwa huo ukulinginisha na miongo kadhaa iliyopita.
Wakimteua kocha Avram Grant  kuchua kikosi cha Ghana zikiwa zimebaki wiki kadhaa kabla mashindano hayajaanza hakuna aliyetegemea kocha huyo kama angefanikiwa kutinga hatua ya fainali, maana hakua akikijua vyema kikosi chake lakini kocha huyo amefanikiwa kukiongoza kikosi hicho mpaka kwenye hatua ya fainali.
Ghana wameonekana kucheza mchezo wa kuvutia kwenye fainali za mwaka huu pamoja na mwanzo mbovu wa kupoteza kwa kufungwa 2-1 na Senegal kwenye mechi yao ya ufunguzi lakini wamekua wakiimarika kutoka mechi moja hadi nyingine. Wakimtumia. Christian Atsu winga wao anae kipiga Chelsea lakini akiwa Everton kwa mkopo ameonekana kung’ara sana kwenye michuano ya mwaka huu.
Lakini pia wana Kwesi Appiah anae cheza kwenye klabu ya Crystal Palace lakini nay eye akiwa Cambridge United kwa mkopo na nyota mwingine Andre Ayew anayeongoza kwa magoli mpaka sasa kwenye michuano hiyo lakini pia mkongwe Asamoah Gyan watakiongoza kikosi cha Ghana leo usiku.
Gyan amekua msaada mkubwa kwa Ghana baada ya kuifungia timu yake magoli muhimu lakini alikosekana kwenye mechi ya ufunguzi kwa kusumbuliwa na malaria wakati timu yake ikilala 2-1 kwa Senegal, na baadae akaikosa nusu fainali akiuguza majeraha ya tumbo baada ya kugongwa na Naby Yattara.
Kwa upande wa Ivory Coast wao wanajivunia kiungo wao wa Manchester City Yaya Toure na mshambuliaji mpya wa klabu hiyo Wilfred Boy, lakini Yaya Toure ameshindwa kuonesha kiwango chake kwenye micuano hii ambacho watu wamezoea kumuonanacho akiwa Man City atakiongoza kikosi cha Ivory Coast leo kusaka ushindi.
Akicheza kama kiungo mkabaji  Toure ameshindwa kunesha makali yake yaliozoeleka lakini amekuwa akisaidiwa na washambuliaji wa timu hiyo kupata matokeo mazuri. Wakiwa na Bony na Gervinho mbele, huku safu yao ya ulinzi ikiongozwa na Kolo Toure Ivory Coast bado wananafasi ya kuchukua ubingwa wa Afrika.
Katika mchezo wa jana wa kumtafuta mshindi wa tatu, timu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ilifanikiwa kuinyuka timu ya Equatorial Guinea goli 4-2 kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya timu hizo kutoka sare ya bila kufungana kwenye muda wa kawaida.

clouds stream