Tuesday 17 February 2015

‘Magaidi’ jijini Tanga Watiwa Mbaroni

‘Magaidi’ jijini Tanga Watiwa Mbaroni

Jeshi la Polisi Tanzania.
Jeshi la Polisi Tanzania lafanikiwa kuwakamata wanaodaiwa kuwa magaidi jijini Tanga.
 Jeshi la Polisi jijini Tanga linawashikilia watu  kadhaa wanaodaiwa  kuhusiana na kikundi cha Ugaidi kilichofanya mashambulizi na jeshi la Polisi na kusababisha kifo cha askari mmoja wa jeshi la Wananchi pamoja na  askari Polisi wengine kujeruhiwa. Akizungumzia tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi  wa Mkoa wa Tanga, Juma Ndaki amesema kuwa jeshi la Polisi linawashikilia watu kadhaa ambao hakutaja idadi yake pamoja na kama ni  wa kikundi cha ugaidi au la.
Amaeongeza kuwa hali katika kitongoji cha Majimoto, Amboni na mkoa wa Tanga kwa ujumla iko shwari na  kusisitiza kuwa  Jeshi la Polisi  linaendelea kufanya uchunguzi kubaini  wahalifu  hao pamoja na silaha zilizoibwa.
Kamanda Ndaki amesema kuwa  hali ni shwari na umma wa Watanzania upuuze taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikitia hofu wananchi kuhusiana na tukio hilo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga,  Magalula Said Magalula amewataka wakazi wa Tanga na vitongoji vyake, kuondoa hofu kwa kuhakikisha wanaendelea na shughuli zao za uzalishaji kwa sababu ulinzi umeimarishwa na hali ya usalama ni  shwari.

clouds stream