Thursday 19 February 2015

Watu wawili wafariki wakijaribu kuiba petroli

Watu wawili wafariki wakijaribu kuiba petroli

Watu wawili wakazi wa Mbeya wamefariki Dunia wakiwa kwenye harakati za kuiba mafuta kwenye Lori lililoacha njia wakati likiwa kwenye safari ya kuelekea Malawi jana tarehe 19.02.2015.
Taarifa za polisi zinasema watu hao ni Maria Pajela, 18, na William Paschal, 38 na wakazi wengine kwenye kijiji hicho waliiba mafuta kwenye kwenye gari lililokuwa limebeba kiasi cha lita 41,000.
Dereva wa gari hilo Zawadi Nyato, 46, na konda wake Bw.Frank Yohana, 24, wote ni wakazi wa Mbeya na wliokolewa na wasamalia na kupelekwa hospitali kupata huduma.
Taarifa zinasema baada ya gari hilo kuanguka wanakijiji walivamia na kuanza kuiba mafuta, majeruhi 18 wamepelekwa kwenye hospitali ya Igongwe.

clouds stream