Tuesday 17 February 2015

Deni la Euro bilioni 240 kuiweka matatani Ugiriki

Deni la Euro bilioni 240 kuiweka matatani Ugiriki

Serikali ya Ugiriki imeleezea imani yake kwamba mkataba kuhusu madeni yake, utafikiwa ndani ya saa arobaini na nane, licha ya kupinga muda wa mwisho uliowekwa na nchi za Ulaya zinazotumia sarafu ya euro.
Mkutano wa mawaziri kutoka nchi za Ulaya zinazotumia sarafu ya euro waliokutana mjini Brussels, Ubalegiji ulivunjika mapema kuliko ulivyotarajiwa wakati serikali ya Ugiriki kutupilia mbali fursa iliyotolewa kwa nchi hiyo hadi Ijumaa kuhusu mpango wa nchi hiyo kudhaminiwa, au kuona mipango ikiisha kufikia mwishoni mwa mwezi huu.
Lakini waziri wa fedha wa Ugiriki, Yanis Varoufakis, amesema Ulaya itafanya “ulaghai uliozoeleka” kwa kutumia mkataba usio na ufumbuzi wa hali iliyopo.
Serikali ya Ugiriki inataka kumaliza masharti iliyowekewa katika deni lake la euro bilioni mia mbili na arobaini. Lakini bila ya fedha za nyongeza kufikia mwishoni mwa mwezi, inaweza kukosa fedha.

clouds stream