Tuesday 24 February 2015

Iringa: Wananchi wapigana na Polisi, kituo cha polisi chachomwa moto

Iringa: Wananchi wapigana na Polisi, kituo cha polisi chachomwa moto

Vurugu zaibuka kati ya Wananchi na Polisi mkoani Iringa leo.
Vurugu zimeibuka mkoani Iringa kati ya wananchi na askari wa jeshi la Polisi katika kituo cha Polisi cha Ilula kufuatia mwanamke ambaye ni mama ntilie kufariki dunia wakati akiwakimbia Polisi waliokuwa katika msako maalumu dhidi ya wafanyabiashara hao.
Kwa mujibu wa mwananchi ambaye hakutaka jina lake liandikwe  kwenye mtandao wa Hivisasa amesema kwamba kifo cha mwanamke huyo kimetokea wakati wa Purukushani hizo ambapo alianguka na kufariki dunia hapo hapo wakati anawakimbia askari hao.
Aidha, inadaiwa kuwa kufuatia tukio hilo Wananchi walipandwa na hasira na kuamua kuvamia kituo cha polisi na kuvunja milango kisha kuwafungulia mahabusu waliokuwemo ndani, wakachoma moto baadhi ya magari yaliyokuwepo kituoni hapo pamoja na mafaili.
Juhudi  za kumtafuta Kamanda wa Polisi mkoani Iringa zinaendelea ili azungumzie tukio hilo.

clouds stream