Friday 13 February 2015

Rais agawa nyumba,fedha kwa wachezaji timu ya Ivory cost

Rais agawa nyumba,fedha kwa wachezaji timu ya Ivory cost

Wachezaji wa Ivorycoast wakishangilia ushindi
Wachezaji wa Ivorycoast wakishangilia ushindi.
Timu ya Taifa ya Ivory coast imelamba dume  imeahidiwa na  kuzawadiwa mamilioni ya dola na Serikali ya nchi hiyo baada ya kutwaa kombe la mataifa Afrika.
Rais Allassane Ouattara amesema  atawapatia wachezaji wote 23, kila mmoja Nyumba yenye thamani ya takriban dola elfu hamsini, na dola elfu hamsini nyingine mkononi  baada ya kuifunga Ghana kwenye fainali za michuano hiyo.
Ghana nayo si haba haijaondoka mikono mitupu kwani Mdhamini wao Shirika la petroli la Taifa atampatia kila mchezaji wa dola elfu 25.

clouds stream