Friday 13 February 2015

Tanzania yaporomoka kwenye viwango vya soka duniani

Tanzania yaporomoka kwenye viwango vya soka duniani

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’
Tanzania imeshuka kwa nafasi tatu katika viwango vya ubora vya shikisho la mpira wa miguu duniani FIFA, Tanzania awali ilikua nafasi ya 104 lakini kwa sasa imeshuka mpaka nafasi ya 107.
Takwimu zilizotolewa jana na FIFA zinaonesha kuwa Tanzania inashikilia nafasi ya 32 kwa upande wa Afrika.
Ivory Coast imepanda katika orodha ya shikisho la soka duniani FIFA baada ya kushinda kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu. Kikosi cha Ivory Coast kimepanda nafasi nane juu hadi nafasi ya 20, lakini Algeria wanaendelea kuongoza kwa kuwa timu bora barani Afrika.
Mataifa kumi bora duniani barani Afrika: 1.Algeria 2.Ivory Coast 3. Ghana 4.Tunisia 5. Cape Verde 6.Senegal 7. Nigeria 8. Guinea 9. Cameroon 10. Congo DR
Mataifa kumi bora duniani: 1. Ujerumani 2. Argentina 3. Colombia 4. Ubeligiji 5. Uholanzi 6. Brazil 7. Ureno 8. Ufaransa 9. Uruguay 10. Hispania
Hakuna timu mpya iliyoingia wala kutoka kwenye orodha ya mataifa 10 duniani, hivyo kufanya orodha ya timu 10 bora duniani kubaki vilevile.

clouds stream