Wednesday 18 February 2015

Bunduki waliyoporwa Polisi yapatikana Mapango ya Amboni Tanga

Bunduki waliyoporwa Polisi yapatikana Mapango ya Amboni Tanga



Jeshi la Polisi jijini Tanga limefanikiwa  kuipata bunduki aina ya SMG, ikiwa na risasi 20 ndani ya mapango ya Majimoto katika eneo la Amboni.
Hatua hiyo inafauatia  msako maalumu uliodumu kwa siku nne sasa, uliolenga kusaka silaha na wahalifu wanaodaiwa kujificha ndani ya mapango ya mawe yaliyopo Amboni, nje kidogo ya mji wa Tanga.
Kwa mujibu wa Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja akizungumza na waandishi wa Habari jijini Tanga jana amesema “Kutokana na taarifa kutoka kwa wananchi Februari 16 mwaka huu katika kitongoji cha la ‘Kona Z’ kilichopo Amboni, tulifanikiwa kumkamata mtu mmoja ambaye kwa sasa sitamtaja jina kwa sababu upelelezi unaendelea, tulimhoji kwa kina akatupa taarifa kuhusu silaha hii,”
Ameongeza kuwa  Jeshi la Polisi  linawashikilia watu kadhaa akiwemo aliyesababisha kupatikana kwa bunduki hiyo. Baadhi ya watu wanaendelea kuhojiwa, kupata taarifa kwa lengo la kukamata waliopora silaha kwa askari na kurushiana risasi kwenye mapango hayo.
Hata hivyo  alikanusha taarifa zilizoenea mjini kwamba ipo miili ya wahalifu,iliyokutwa ndani ya mapango hayo, kutokana na mapigano yaliyofanyika mwishoni mwa wiki

clouds stream