Thursday 26 February 2015

Walemavu wa ngozi kuitikisa Ruvuma kwa maandamano

Walemavu wa ngozi kuitikisa Ruvuma kwa maandamano


Watu wenye ulemavu wa ngozi Albino waendelea kuishi maisha ya hofu nchini Tanzania.
Watu wenye ulemavu wa ngozi Albino waendelea kuishi maisha ya hofu nchini Tanzania.
Maandamano makubwa kupinga mauaji pamoja na unyanyasaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) yanatarajiwa kufanyika mkoani Ruvuma machi 2 mwaka huu.
Kwa mujibu wa  katibu mtendaji wa chama cha walemavu wa ngozi mkoa wa Ruvuma, Amini Mapunda amesema kwamba lengo la maandamano hayo ni   kuishinikiza serikali kuwachukulia hatua kali wote waliohusika na kubainika na tuhuma za kuhusika na mauaji ya albino kwa madai kwamba baadhi yao wamekamatwa lakini mwenendo wa kesi zao bado haueleweki.
Mauaji ya Albino  pamoja  na wazee  nchini  Tanzania  yamekuwa yakihusishwa na imani za kishirikina, utajiri ama nafasi  mbalimbali za kisiasa kwa imani za kishirikina huku serikali ikishindwa  kuchukua hatua kali kwa wahusika suala linalopelekea mauaji hayo kuendelea.
Kwa upande wake  mwenyekiri wa shirika la ROA, Mathew  Ngalimanayo  amesema kuendelea kwa mauaji hayo   inatokana na jamii kukosa hofu ya mungu na wakati mwingine  familia husika zikihusika kutokana na hali ngumu ya maisha hivyo kushawishika kirahisi.

clouds stream