Saturday 7 February 2015

Chelsea yazidi kusogelea ubingwa


Chelsea yazidi kusogelea ubingwa


Kiungo wa Chelsea Eden Hazard akishangilia baada ya kufungia bao timu yake
Kiungo wa Chelsea Eden Hazard akishangilia baada ya kuifungia bao timu yake

Chelsea imeendelea kujiimarisha  kileleni mwa ligi kuu ya Uingereza baada ya ushindi wao wa magoli 2-1 dhidi ya Aston Villa kwenye uwanja wa Villa Park kwenye mchezo wa ligi kuu nchini humo.
Eden Hazard alliandikia Chelsea bao la kwanza dakika ya nane lakini Jores Okore alisawazisha goli hilo dakika ya 48kwa kufunga goli murua kwa kichwa.
Branislav Ivanovic aliifungia Chelsea goli la pili na na ushindi dakika ya 66 na kua shujaa wa mchezo kwa upande wa timu yake. Ushindi huo unaifanya Chelsea iongoze ligi kwa tofauti ya pointi saba mbele ya Man City waliolazimishwa sare ya 1-1 na Hull City.

clouds stream