Thursday 12 February 2015

NEC, Vyama vya siasa wajadili maboresho daftari la wapiga kura

NEC, Vyama vya siasa wajadili maboresho daftari la wapiga kura

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva akitoa taarifa kwenye mkutano na vyama vya siasa.
Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva akitoa taarifa kwenye mkutano na vyama vya siasa.
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe (kulia) na katibu mkuu wa Chadema Wilbroad Slaa katika mkutano na    Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe (kulia) na katibu mkuu wa Chadema Wilbroad Slaa katika mkutano na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba.
Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye(kushoto)
Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye(kushoto).
Dar es salaam, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)  leo   imekutana  na viongozi wa vyama siasa jijini Dar es salaam. Katika mkutano huo Tume ya Taifa imetoa tathimini ya zoezi la majaribio  la Uboreshwaji wa Daftari la Kudumu  la Wapigaji kura katika majimbo ya  majaribio.
Aidha, majimbo ya majaribio ambayo tume ya Taifa ya Uchaguzi imeandikisha kwa kutumia teknolojia ya Biometric Voter Registration  (BVR) ni  Kawe, Dare s salaam, Kilombero Morogoro, pamoja  na  Milele mkoani Katavi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Tume, Julias Maluba amesema kuwa maandalizi mengine waliyofanya ni pamoja na uhakiki wa vituo vya kuandikishia wapiga kura, katika ngazi ya vitongoji, vijiji na mitaa, hivyo tume imefanikiwa kuongeza vituo vingine vipya kutoka vituo 24,919 hadi vituo 36,109 vya sasa.
Akizungumzia  changamoto Malaba amesema kuwa ni pamoja na ‘setting’ za mashine inayotumika katika zoezi hilo la uchukuaji wa alama za vidole na  majina ya wenye alama.
Mkutano huo umejiri kufuatia vyama vya upinzani kuilaumu tume hiyo kwa kutowashirikisha kama ambavyo waliahidiwa na tume hiyo kabla ya kuanza zoezi la uandikishaji.

clouds stream