Thursday 19 February 2015

Kituo cha Polisi Vingunguti chazinduliwa leo

Kituo cha Polisi Vingunguti chazinduliwa leo

Kituo kidogo cha Polisi  Vingunguti  kimezinduliwa  leo jijini Dar es salaam ambapo mamia ya wananchi wamehudhuria  katika tukio hilo.
Aidha, Kituo  hicho kimezinduliwa na Kamanda wa kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova. Hatua inafuatia eneo la vingunguti kutokuwa na kituo cha polisi kwa muda mrefu suala lilipelelekea kukithiri kwa vitendo uhalifu.
Nao wananchi wamelipongeza jeshi la Polisi nchini Tanzania kwa kujenga kituo hicho suala ambalo litapelekea  kudhibiti uhalifu  pamoja na  kuimarisha  ulinzi wa  mali za wa wananchi.

clouds stream