Saturday 7 February 2015

Mbunge, walinzi wake wauawa kwa kupigwa risasi nchini Kenya

Mbunge, walinzi wake wauawa kwa kupigwa risasi nchini Kenya

Gari la Mbunge wa jimbo la Kabete  George Muchai aliyepigwa risasi.
Gari la Mbunge wa jimbo la Kabete George Muchai aliyepigwa risasi.
Matundu ya risasi iliyopigwa na wauaji.
Matundu ya risasi iliyopigwa na wauaji.
Jeshi la Polisi likipima eneo la tukio.
Jeshi la Polisi likipima eneo la tukio.
Ndugu wa Mbunge akilia kwa uchungu kufuatia ndugu yake kuuawa.
Ndugu wa Mbunge akilia kwa uchungu kufuatia ndugu yake kuuawa.
Mbunge  wa jimbo la Kabete Bw. George Muchai ameuawa kwa kupigwa  risasi leo asubuhi  katika barabara ya Uhuru.Tukio hilo limetokea  leo kati  ya saa tisa  na saa kumi na nusu usiku wa kuamkia leo.
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi  Nairobi Kati OCPD Paul Wanjama  amesema katika tukio hilo walinzi wawili wa Mbunge huyo na  dereva  nao wameauawa kwa kupigwa risasi.
Akizungumzia tukio hilo dereva aliyeshuhudia tukio hilo alisema kwamba gari la mbunge huyo lilisimama katika eneo la Mzunguko (roundabout) ambapo watu nne walitokea wakiwa na bunduki  na kuanza kuwashambulia.
Ameongeza kuwa waliwamininia risasi nyingi na hatimaye kutoweka. Baada ya muda walifika katika eneo la tukio ambapo mbunge huyo akiwa na wenzake tayari walikuwa  wameuawa.
Naye muuza magezeti aliyeshuhudia tukio hilo aliwaambia Polisi kuwa mmoja wa wauaji hao alikuwa amejifunika usoni (mask). Miili ya Mbunge na pamoja na walinzi walio uawa imeonekana kuwa na matundu ya risasi kichwani pamoja na kifuani ambapo imepelekwa  katika maeneo ya Lee nchini Kenya.
Katika hatua nyingine Seneta wa Kiambu Bw. Kimani Watamangi amesema Bw. Muchai alikuwa anatishiwa mara kadhaa na aliwahi kuripoti katika jeshi la Polisi nchini humo.

clouds stream