Saturday 7 February 2015

Waziri mkuu ahirisha rasmi Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Waziri mkuu ahirisha rasmi Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Waziri mkuu Mizengo avunja  Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Waziri mkuu Mizengo avunja Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Waziri Mkuu  Mizengo Pinda leo amevunja rasmi  Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania mjini Dodoma. Bunge hilo limefanya vikao  kwa muda wa siku 12 hadi leo jumamosi.
Akihutubia kabla ya kuvunja Bunge hilo Pinda amesema kwamba Tanzania ina ziada ya tani Milioni 3.2 za chakula kutokana na uzalishaji wa mazo ya chakula msimu wa 2013/2014 kufikia jumla ya tani milioni 16.0 wakati makadirio ya mahitaji ya chakula kwa mwaka 2014/2015 ni tani milioni 12.8.
Ameongeza kuwa Tanzania imeweza kujitosheleza kwa chakula kwa asilimia 125 suala ambalo linatokana na Mpango wa Kilimo kwanza ambao umeongeza tija katika uzalishaji.
Katika mkutano wa 18 wa Bunge la Jamhuri,jumla ya maswali 122 ya msingi na 313 ya nyongeza yaliulizwa na wabunge  na maswali 15 ya msingi kwa waziri mkuu  na nyongeza 13 yaliulizwa. Mkutano huo umeahirishwa hadi marchi 17 mwaka huu katika mkutano mwingine  wa 19.

clouds stream