Thursday 19 February 2015

Southampton wasajili mchezaji wa Uganda

Southampton wasajili mchezaji wa Uganda


amugabi
Baada ya kusajili mchezaji kutoka Kenya Victor Wanyama sasa timu hiyo ya ligi kuu ya Southampton nchini Uingereza imeamia nchini Uganda na sasa ni kijana wa miaka 19, Bevis Kristofer Kizito Mugabi kwa mkataba wa miaka miwili na nusu.
Mlinzi huyo licha ya wazazi wake wote wawili kuwa ni waganda bado ana uraia wa nchi mbili ambazo zinampa nafasi ya kuchezea timu ya taifa ya Uganda kwakuwa bado hajachezea timu ya wakubwa ya Uingereza.
Akiongea kwenye mtandao wa timu amesema amefurahi kujiunga na klabu hiyo baada ya timu ya awali ya Fulham kumuacha kwenye msimu wa 2011.
“Nimefurahi kupata nafasi hii, nimesaini na kila kitu kimekamilika. Lengo langu ni kucheza katika kikosi cha kwanza. Nitafanya kazi kwa bidii mazoezini na wakati wa mechi,” amesema beki huyo mwenye umri wa miaka 19.

clouds stream