Thursday 19 February 2015

Boko Haram 300 wauawa Nigeria ?

Boko  Haram 300 wauawa  Nigeria ?

Jeshi la Nigeria limesema kuwa limewaua zaidi ya wapiganaji 300 wa Boko Haram, baada ya jeshi la nchi hiyo kukomboa tena miji kadhaa iliyotekwa na wapiganaji hao kazkazini mashariki mwa Monguno.
Msemaji wa jeshi Chris Olukolade amesema kuwa wapiganaji wachache wa kiislamu pia wamekamatwa.
Mataifa kadhaa ya magharibi mwa Afrika kama vile Niger, Chad na Cameroon, ambayo yanakabiliana na Boko Haram pia yametoa taarifa ya maafa makubwa kwa kundi hilo ambalo limeleta kero kubwa katika ukanda huo.
Siku ya jumatatu wiki hii jeshi la Nigeria lilisema kuwa limeutwaa tena mji wa Monguno, ambao ulikuwa umetekwa na wapiganaji hao wa jihadi mwezi uliopita.

clouds stream