Saturday 7 February 2015

Umoja wa mataifa kuchukua hatua Yemen

Umoja wa mataifa kuchukua hatua Yemen


Raia wa Yemen waandamana kupinga waasi wa Houthi .
Raia wa Yemen waandamana kupinga waasi wa Houthi .
Baraza la usalama la umoja wa mtaaifa limesema kuwa liko tayari kuchukua hatua zaidi iwapo waasi wa Houthi hawawezi kurudi katika meza ya mazungumzo mara moja kwa ajili  ya kufanya  mazungumzo  ya kidemokrasia.
Kundi hilo linalodhibiti mji mkuu wa Sanaa limevunja bunge na kuteua baraza la mpito kuchukua madaraka.
Wanachama wa baraza la usalama wanasema kuwa pande zote ni lazima zirejee kwenye mazungumzo ya umoja wa mataifa ambapo walitaka kuachiliwa mara moja kwa rais wa Yemen, waziri mkuu na baraza la mawaziri kutoka vizuizi vya nyumbani.
Nchi za ghuba zimekuwa zikiomba hatua zaidi kutoka kwa jamii ya kimataifa dhidi ya mzozo ulio nchini Yemen.

clouds stream