Monday 9 February 2015

Uchaguzi wa Rais Nigeria ‘ Kizungumkuti ‘

Uchaguzi wa Rais Nigeria ‘ Kizungumkuti ‘

Uchaguzi wa Nigeria
Uchaguzi wa  Rais  Nigeria bado ni kitendawili.
Tume ya uchaguzi ya Nigeria imekutana na waakilishi wa vyama vyote vya siasa vilivyoandikishwa kujadiliana iwapo uchaguzi mkuu wa Jumamosi (14/02/15) utafanyika au  kuarishwa.
Rais Goodluck Jonathan, magavana wa majimbo, wakuu wa jeshi, na ma-rais wa zamani, wameiomba tume ya uchaguzi ijadili na pande zote kuhusu hali ya usalama nchini.
Katika hatua  nyingine  kundi la wapiganaji Waislamu, Boko Haram, linafanya mashambulio makali kaskazini-mashariki mwa Nigeria ambako linadhibiti eneo kubwa.

clouds stream