Monday 16 February 2015

Tanga: Mwanajeshi 1 auawa, askari Polisi 4 wajeruhiwa katika mapigano na kikundi cha kigaidi

Tanga: Mwanajeshi 1 auawa, askari Polisi 4 wajeruhiwa katika mapigano na kikundi cha kigaidi



Askari mmoja wa jeshi la wananchi ameuawa kwa kupigwa risasi huku wengine wanne wa jeshi la polisi wamejeruhiwa vibaya na kulazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa tanga Bombo kufuatia mashambilizi ya kurushiana risasi katika mapango kati yao na vikundi vinavyodaiwa kuwa vya kigaidi.
Kwa mujibu wa  kamishna wa Polisi -Operesheni na mafunzo Paul Changonja akielezea tukio hilo amekiri kuwa askari wake watatu na mmoja wa jeshi la wananchi wamejeruhiwa kwa risasi wakati askari wake walipoingia katika mapango kukabilina na kikundi kikundi cha kigaidi kinachodiwa kupora polisi silaha hivi karibuni.
Ameongeza kuwa mapambano hayo yalitokea muda mfupi tu wakati wa msako maalum wa kutafuta silaha zinazodaiwa kufichwa kwenye moja ya eneo la mapango ya Amboni, yaliyoko umbali wa kilometa 10 kutoka katikati ya Jiji la Tanga.
Kujeruhiwa kwa  askari hao kumetokana na mapambano ya kurushiana risasi yaliyodumu kwa dakika 15 alfajiri ya kuamkia jana katika mashimo ya mawe ambayo yako jirani na mapango ya Amboni.
Kamishna Chagonja alisema baada ya kuzima mapigano, waliamua kuingia ndani ya mapango hayo na kukuta vifaa mbalimbali vya kutengenezea milipuko, pikipiki moja, baiskeli tatu, silaha mbalimbali za jadi ikiwemo mishale, pinde , visu na mapanga lakini hawakufanikiwa kukuta mtu.
Katika hatua nyingine tukio hilo limesababisha hofu kubwa miongoni mwa wananchi jijini Tanga.

clouds stream