Monday 16 February 2015

Urais 2015: CUF yamteua Prof. Lipumba kugombea urais

Urais 2015: CUF yamteua Prof. Lipumba kugombea urais

Dares salaam, Hatimaye Chama cha wananchi CUF leo kimetangaza kupeleka  jina la Mwenyekiti wa Chama cha CUF Prof. Ibrahim Lipumba katika umoja wa katiba ya wananchi UKAWA. Jina hilo litaunganishwa na majina ya wanachama wengine katika umoja wa katiba ya wananchi achaguliwe kuiwakilisha Ukawa ambapo  atapambana na kada kutoka chama tawala cha Mapinduzi (CCM).
Kwa mujibu wa Naibu mkurugenzi wa uchaguzi wa chama cha wananchi CUF Bwana Shaweji Mketo amesema kuwa  kwa mujibu wa makubaliano na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi kila chama kitateua mgombea katika nafasi zote na kisha kushindanisha ili kupata mgombea moja atakayeungwa mkono na vyama vyote.
Ameongeza kuwa  katika nafasi ya viti vya udiwani na ubunge kwa wanaotaka kugombea fomu zitaanza kutolewa kuanzia machi 1 hadi 10 kupitia makatibu wa matawi na katika nafasi ya ubunge wagombea watatakiwa kuchukua fomu kwa makatibu kata na kuzirudisha kwa makatibu wa wilaya.
Katika hatua nyingine   amesisitiza  kuwa  aprili 17 hadi 19 kurugenzi ya uchaguzi inatarajia kukaa na kufanya mchujo kwa wagombea ubunge

clouds stream