Monday 9 February 2015

Watu sita wafariki kwa ajali moto Dar es salaam

Watu sita wafariki kwa ajali moto Dar es salaam

Nyumba iliyoteketea kwa moto.
Nyumba iliyoteketea kwa moto.
Ndugu wakilia kwa uchungu kufuatia ndugu kufariki dunia kwa ajali ya moto.
Ndugu wakilia kwa uchungu kufuatia ndugu kufariki dunia kwa ajali ya moto.
Ilala, watu sita wamefariki dunia  kwa ajali ya moto iliyotokea katika eneo la Kipunguni A, Ukonga Banana.Waliofariki dunia katika ajali hiyo ni pamoja Kapteni mstaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi(JWTZ).
Akizungumzia tukio hilo  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Mary Nzuki alisema kuwa moto huo ulizuka ghafla katika nyumba inayomilikiwa na mstaafu huyo wa Jeshi, David Mpira anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 55 na 60  jana saa 10:30 alfajiri.
Aliwataja  wengine waliokufa katika ajali hiyo ni mke wa marehemu, Selina Yegela anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 50 na 55, ambaye pia ni mstaafu wa iliyokuwa Kampuni ya Kuhudumia Ndege (DAHACO), sasa Swissport.
Aidha, moto huo pia umesababisha vifo vya watoto wawili wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 na 30 ambao ni, Lucas Mpira na Samwel Yegela.
Kamanda Nzuki alisema wajukuu wa marehemu nao wamekufa katika ajali hiyo, ambao ni Selina Emmanuel (9) mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Minazi Mirefu na Pauline Emmanuel (3), mwanafunzi wa chekechea katika Shule ya Tumaini iliyopo Kitunda.
Chanzo  cha moto huo bado  hakijajulikana ambapo hadi sasa  maiti zimehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na uchunguzi bado unaendelea.

clouds stream