Friday 13 February 2015

Kocha wa Aston Villa atimuliwa kazi

Kocha wa Aston Villa atimuliwa kazi


258D730C00000578-0-image-a-3_1423684946380
Kocha wa Aston Villa Paul Lambert ametimuliwa kazi baada ya timu yake kushindwa kufanya vizuri kwa kupokea vipigo mara kwa mara,huku ikiwa imefunga magoli 12 tu kwenye mechi 25 ilizocheza ikiwa ni moja ya rekodi mbovu kuwahi kutokea.
Aston Villa kwa sasa inashika nafasi ya 18 kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza baada ya kupoteza mechi 10 mfululizo.
_80948859_astonvillabannerpa
Mashabiki waliendelea kushinikiza uongozi wa klabu kumfukuza kocha huyo baada ya kupata kipigo cha 2-0 mbele ya Hull City mpaka Gazeti la Birmingham Mail kuanzisha kampeni inayosema “Lambert Must Go!”. Mkurugenzi wa Aston Villa,Tom Fox aliongea na BBC na kuonyesha dhamira yake ya kumpa muda kocha wake na jukumu la kumfukuza ni la haraka zaidi.
Paul-Lambert-has-been-put-008
Paul Lambert alijiunga na Aston Villa baada ya kufanya vizuri kwenye vilabu vya Livingston, Wycombe, Colchester na Norwich na pia alifanikiwa kuipandisha timu ya daraja la chini ya Canaries mpaka ligi kuu na alifanikiwa kushika nafasi ya 15 kwa misimu miwili mfululizo.

clouds stream