Tuesday 10 February 2015

Viingilio vya mechi ya Yanga dhidi ya BDF hivi hapa

Viingilio vya mechi ya Yanga dhidi ya BDF hivi hapa



Afisa Habari wa Yanga Jerry Muro
Afisa Habari wa Yanga Jerry Muro

Klabu ya Yanga imetangaza viingilio vyao katika mechi yao ya kwanza ya kombe la Shirikisho dhidi ya wageni wao timu ya BDF XI ya Botswana kwenye uwanja wa Taifa ambapo kiingilio cha chini kabisa kitakua ni shilingi 5000.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha Yanga, Jerry Muro amesema wameamua kuweka kiwango hicho lengo likiwa ni kuwavuta mashabiki na wapenzi wa soka wengi kuja kuishangilia timu yao wakati itakapokua inacheza na wapinzani wao BDF XI.
Viingilio vingine kwenye mchezo huo vitaku ni shilingi 10000 kwa jukwaa la viti vya rangi ya chungwa, VIP C itakua ni shilingi 15000, VIP B shilingi 20000 wakati VIP A itakua ni shilingi 30000.
“Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wasitarajie kuuona mchezo huo kupitia luninga, maana hatuta ruhusu hilo na badala yake fursa hiyo wataipata wale wakazi wa mikoni kuuona mchezo huo kupitia luninga lakina wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam hawatapata matangazo hayo hivyo wanashauriwa waje uwanjani,” alisema Muro.
Tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa mapema, tutaanza kuuza siku moja kabla ya mchezo lakini pia tutoe taarifa fupi kuhusu hali ya kikosi chetu, tulikua na wachezaji wawili ambao walikua majeruhi kipa wetu Deogratius Munishi ‘Dida’ na kiungo Haruna Niyonzima kwa sasa wapo safi tayari kwa mazoezi.

clouds stream