Tuesday 24 February 2015

Julio atua Coastal Union kutoa msaada

Julio atua Coastal Union kutoa msaada

Kocha wa Mwadui FC Jamhuri Kihwelo Julio, amejiunga na kikosi cha Coastal Union kwa ajili ya kutoa msaada wa kiufundi
Kocha wa Mwadui FC Jamhuri Kihwelo Julio, amejiunga na kikosi cha Coastal Union kwa ajili ya kutoa msaada wa kiufundi
Kocha wa klabu ya Mwadui FC ya mjini Shinyanga Jamhuri Kihwelo Julio ‘Pereira’ amejiunga na timu ya Coastal Union ya jijini Tanga kwa ajili ya kutoa msaada wa kiufundi kwenye benchi la ufundi la timu hiyo kutokana na timu hiyo kusuasua kwenye ligi kuu Tanzania Bara.
Julio ambaye amefanikiwa kuipamdisha daraja Mwadui FC na pia kuipa ubingwa wa ligi daraja la kwanza ametua kwenye kikosi cha Coastal Union kwa ajili ya kushirikiana na kocha mkuu wa timu hiyo Mkenya James Nandwa ili kusaidiana kwa kuhakikisha inafanya vizuri kwenye michezo iliyobaki.
Julio amesema Coastal ni timu yake na akiwa hapo anajiona yupo nyumbani na amewaahidi mashabiki na wapenzi wa Coastal watarajie mambo mazuri kutoka kwake akishirikiana na kocha mkuu wa timu hiyo.
“Coastal ni timu yangu na wameniomba nije nitoe msaada, kuanzia sasa timu itatisha maana mgonjwa kapata daktari wapenzi na mashabiki wasubiri raha. Nimesha maliza kujenga daraja Mwadui nimekuja kupandisha ghorofa Coastal,” ametamba Julio.
Kwa siku za hivi karibuni, timu ya Coastal Union imekua na matokeo mabovu na ilipoteza mchezo wake wa mwishoni mwa wiki iliyopita mbele ya Ndanda FC kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

clouds stream