Monday 9 February 2015

Necta yawatoa hofu wananchi kuhusu matokeo ya kidato cha nne

Necta yawatoa hofu wananchi kuhusu matokeo ya kidato cha nne


Katibu mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde.
Katibu mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde.
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limesema usahihishaji wa mitihani ya kidato cha nne uliofanyika Novemba mwaka jana, umekamilika. Hatua hiyo inafuatia baadhi ya wanafunzi waliomaliza kidato cha nne kuwa na shauku ya kutaka kufahamu walichovuna kutokana na kukaa  darasani kwa miaka takribani minne.
Kwa mujibu wa  Katibu mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema kuwa usahihishaji umekamilika na baraza lipo katika uchambuzi wa kuyapanga na yatakapokamilishwa watayatangaza.
Aidha, Katika kipindi cha miaka miwili mfululizo, mwaka 2012 na 2013, Necta ilitangaza matokeo ya kidato cha nne mwishoni mwa Februari na mwanzoni mwa Machi.
Katika  hatua niyinge  muhula wa masomo kwa kidato cha tano huanza Julai, huku  mwezi  Machi na Aprili mchakato wa kuwapangia shule hufanyika wakati Mei na Juni hutumiwa kwa maandalizi ya kuripoti shule  wanafunzi waliofaulu mtihani huo.

clouds stream